The United Republic of Tanzania
Ministry of Energy

WIZARA YA NISHATI YAWASILISHA...

WIZARA YA NISHATI YAWASILISHA UTEKELEZAJI WA HOJA ZA KAMATI YA BUNGE KUHUSU SEKTA NDOGO ZA NISHATI.

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, Novemba 4, 2026, amewasilisha mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini taarifa kuhusu utekelezaji wa hoja mbalimbali zilizotolewa na Kamati hiyo kuhusu miradi inayotekelezwa nchini katika sekta ndogo za Umeme pamoja na Mafuta na gesi,

Uwasilishaji huo umefanyika kufuatia kikao cha Kamati kilichofanyika Oktoba 22, 2026, ambapo Wizara ya Nishati ilielekezwa kuwasilisha majibu na ufafanuzi kuhusu hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali pamoja na masuala mengine yaliyobainishwa na Kamati hiyo.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Bw. Petro Lyatuu, Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Nishati; Mhandisi Innocent Luoga, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati; Bw. Lazaro Twange, Mkurugenzi wa TANESCO, pamoja na wataalamu kutoka taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati.