Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

​BYABATO AHUDHURIA MKUTANO WA...

​BYABATO AHUDHURIA MKUTANO WA NGAZI YA JUU WA JOTOARDHI NCHINI EL SALVADOR

BYABATO AHUDHURIA MKUTANO WA NGAZI YA JUU WA JOTOARDHI NCHINI EL SALVADOR*

Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato amedhuria Mkutano wa Pili wa Ngazi ya Juu wa Jotoardhi _(2nd High Level Conference of the Global Geothermal Alliance), uliofanyika tarehe 30 Septemba, 2022 katika mji wa San Salvador, nchini El Salvador.

Mkutano huo umehusisha Mawaziri, viongozi wa juu wa Serikali, Wabia wa Maendeleo, Taasisi na Sekta Binafsi.

Mkutano huo pamoja na mambo mengine, ulijadili fursa na changamoto katika uendelezaji wa Jotoardhi kwa ajili ya kuzalisha umeme na miradi ya matumizi mengine (direct heat uses) ikitiliwa mkazo katika Sekta ya Kilimo na kuongeza usalama wa chakula.

Mkutano huo umeandaliwa na International Renewable Energy Agency (IRENA), Serikali ya El Salvador kwa kushirikiana na International Geothermal Association (IGA)