MAMA MANYEMA AONGOZA MAPINDUZI YA NISHATI SAFI KWA WAFANYABIASHARA WA CHAKULA.
Mkurugenzi wa Nishati Safi ya Kupikia, Bw. Nolasco Mlay, amempongeza Bi. Afua Juma maarufu kama Mama Manyema, kwa kuhamiakwenye nishati safi ya kupikia katika shughuli zake za biashara, akieleza kuwa hatua hiyo ni mfano mzuri wa uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi kwa wafanyabiashara wa chakula na wananchi wengine kwa ujumla.
Amesema uamuzi wa Mama Manyema kuhamia kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia unaonesha umuhimu wa teknolojia hizo katika kuboresha mazingira ya kazi, kulinda afya ya watumiaji pamoja na kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa shughuli za kiuchumi.
Bw. Mlay amewataka wafanyabiashara wengine wa chakula kuiga mfano huo wa kutumia nishati safi ya kupikia, akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha nishati hiyo inapatikana kwa urahisi kwa wananchi wote.