Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

MRAMBA AWASILI NCHINI AFRIKA K...

MRAMBA AWASILI NCHINI AFRIKA KUSINI KUSHIRIKI JUKWAA LA NISHATI AFRIKA 2025

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felichesm Mramba amewasili nchini Afrika ya Kusini kushiriki Jukwaa la Nishati Afrika 2025 ambalo litaangalia masuala mbalimbali ya Nishati ikiwemo Nishati Safi ya Kupikia. Jukwaa hilo linaanza leo Juni 17,2025 na linatarajiwa kumalizika Juni 20,2025.

Nchini Afrika Kusini, Mhandisi Mramba ameambata na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Mhandisi Innocent Luoga na Mkurugenzi wa Nishati Safi ya Kupikia kutoka Kitengo cha Nishati Safi ya Kupikia Wizara ya Nishati Bw. Nolasco Mlaysambamba na wataalam kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji(EWURA).