The United Republic of Tanzania
Ministry of Energy

NANENANE 2026: LEO AGOSTI 4, W...

NANENANE 2026: LEO AGOSTI 4, WIZARA YA NISHATI YAENDELEA KUHUDUMIA WANANCHI.

Wataalam wa Wizara ya Nishati wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Banda la Wizara ya Nishati katika Maonesho ya NaneNane yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John Samuel Malecela, Nzuguni, jijini Dodoma.

Wizara inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala ya umeme, mafuta, gesi asilia, nishati safi ya kupikia pamoja na fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta ya nishati.

Unapotembelea Maonesho ya NaneNane, karibu utembelee Banda la Wizara ya Nishati na taasisi zake lililopo Government Pavilion Na. 2.