The United Republic of Tanzania
Ministry of Energy

NISHATI NI MBABE DHIDI YA RAS-...

NISHATI NI MBABE DHIDI YA RAS-DSM KATIKA MPIRA WA PETE – SHIMIWI

Timu ya wanawake ya Wizara ya Nishati imeibuka na ushindi wa mabao 15-12 dhidi ya RAS-Dar es Salaam katika mchezo wa mpira wa pete uliochezwa leo, Septemba 25, 2026, katika viwanja vya CCP mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, wakati michuano ya SHIMIWI ikiendelea.

Mwalimu wa timu hiyo, Damian Mchonya, amesema timu yake inaendelea kufanya vizuri na kupata matokeo katika michuano hiyo yenye ushindani, akieleza kuwa ushindi dhidi ya RAS-Dar es Salaam umeongeza matumaini ya kufanya vizuri zaidi katika hatua zinazofuata.

Kwa upande wake, nahodha wa timu hiyo, Juliana Peter, amesema malengo yao ni kuendelea kufanya vizuri, kufuzu hatua ya 16 bora na hatimaye kutinga fainali ya michuano ya SHIMIWI inayoendelea mkoani Kilimanjaro.