NISHATI YAICHAPA WAZIRI MKUU – SERA, BAO MOJA KWA BUYU
Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Nishati imeendeleza imeendeleza ubabe katika michuano ya SHIMIWI baada ya kuicharaza timu ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu kwa bao 1-0.
Mchezo huo umechezwa Septemba 25, 2026, katika viwanja vya Shule ya Msingi Mwelesi vilivyopo mkoani Kilimanjaro.
Ushindi huo umekuja siku moja baada ya timu hiyo kuibuka na ukidedea kwa ushindi wa mabao 2 kwa sifuri dhidi ya timu ya Bunge, na hivyo kuifanya Nishati kuwa katika nafasi nzuri kwenye michuano hiyo.
Mwenyekiti wa Timu ya Michezo ya Wizara ya Nishati, Ndaisenga Rodgers, amesema lengo la timu zote za wizara hiyo ni kuwa mabingwa kwa kuibuka na ushindi mnono katika mashindano hayo.
Aidha, Kocha Mkuu wa timu hiyo Thabiti Manoti ametoa shukrani kwa uongozi wa Wizara ya Nishati kwa kuruhusu wachezaji kushiriki michuano hiyo, akisema hatua hiyo imewapa morali ya kufanya vizuri na kupambana kiume katika michezo yao.
Timu ya Wizara ya Nishati inaendelea na safari yake katika michuano ya SHIMIWI ikiwa *imepangwa Katika kundi D katika hatua za makundi*