Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

​Rais Samia kushuhudia ujazaji...

​Rais Samia kushuhudia ujazaji maji Bwawa Umeme la Julius Nyerere

Rais Samia kushuhudia ujazaji maji Bwawa Umeme la Julius Nyerere

Waziri wa Nishati, Mhe.January Makamba amewaeleza watanzania kuwa, zoezi la kuanza kujaza maji katika Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) litaanza tarehe 22 Desemba 2022 na kushuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Watanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Makamba amesema hayo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo Desemba 18, 2022 mkoani Pwani ambapo alisema kuwa hiyo ni hatua kubwa, muhimu na ya kihistoria katika kutekeleza mradi huo.

Amesema kuwa, mradi huo kwa umefikia asilimia 78 ya utekelezaji wake tangu kuanza kwake.

Alisema kuwa, kutokana na ukubwa wa zoezi hilo na umuhimu wa mradi huo kitaifa, ni ishara kuwa ndoto za Taifa katika kutekeleza mradi huo zinatimia ambapo zoezi hilo litazinduliwa na kushuhudiwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Tunayo faraja kubwa kwamba mjadala ambao umekuwa ukiendelea kuhusu dhamira ya Serikali kukamilisha mradi huo angalau utaondoka sasa baada ya kufikia hatua hii, kwa sababu huu ni ushahidi tosha kwamba Serikali, Rais, Wizara ya Nishati, na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) tumefanya kazi kubwa ya kutekeleza mradi huu kwa nguvu, maarifa na juhudi kwa wakati wote, mahali tulipo fika sasa ni pa kujivunia,” alisema Makamba

Alifafanua kuwa, handaki la kuchepusha maji lina urefu wa mita 700, yaani viwanja saba vya mpira wa miguu na lilijengwa miaka mitatu iliyopita kwa gharama ya shilingi takribani Bilioni 235.

Bwawa hilo pia litakuwa ni kivutio cha watalii kwakuwa liko ndani ya hifadhi na litabadili kabisa taswira ya hifadhi hiyo na thamani ya hifadhi hiyo itaongezeka ndani na nje ya Tanzania.

Tanzania (TANESCO), Maharage Chande aliweka wazi kuwa inakadiriwa kuwa misimu miwili ya kipindi cha mvua, itaweza kujaza maji katika bwawa hilo.

“Tunaanza kujaza maji mwezi huu wa Desemba ambapo kuna mvua za vuli, pia tunategemea mvua za masika mwezi Machi 2023, ambazo zitakuwa mvua za msimu wa kwanza, pia tutapata vuli ndani ya kipindi hicho, kisha tutapata zile za masika katika mwaka 2024 pamoja na vuli ya kipindi hicho, hivyo mvua mbili kubwa za masika zinaweza kujaza bwawa kwa hesabu zilizopo,” Alisisitiza Chande.

Zoezi hilo litahudhuriwa na watu takribani 2000 na litatangazwa moja kwa moja kupitia vyombo vya habari ili watanzania wote waweze kushuhudia maendeleo na hatua iliyofikiwa katika kutekeleza mradi huo.