Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

​TANZANIA NA JICA KUSHIRIKIANA...

​TANZANIA NA JICA KUSHIRIKIANA KATIKA KUJENGA UWEZO WA MATUMIZI BORA YA GESI ASILIA

TANZANIA NA JICA KUSHIRIKIANA KATIKA KUJENGA UWEZO WA MATUMIZI BORA YA GESI ASILIA

Wizara ya Nishati pamoja Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) wamesaini makubaliano ya kutekeleza mradi wa kujengea uwezo Wataalam wa Wizara na Taasisi zake katika eneo la kuendeleza matumizi bora ya Gesi Asilia ili kuiwezesha Tanzania kuendelea kunufaika kiuchumi na rasilimali hiyo.

Makubaliano hayo yamesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba na Mwakilishi Mkuu wa JICA Tanzania, ARA Hitoshi tarehe 16 Mei, 2023 jijini Dar es Salaam.

Makubaliano hayo yatapelekea wataalam wa Tanzania kuongeza ufanisi katika kufanya mipango na kutekeleza miradi ya matumizi ya Gesi Asilia kwa kuzingatia pia suala la utunzaji wa mazingira.