The United Republic of Tanzania
Ministry of Energy

WAANDISHI WA HABARI WAPATA ELI...

WAANDISHI WA HABARI WAPATA ELIMU YA MIRADI YA NISHATI NANENANE.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wametembelea Banda la Wizara ya Nishati katika Maonesho ya NaneNane yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John Samuel Malecela, Nzuguni, jijini Dodoma.

Mara baada ya kutembelea banda hilo waandishi hao wameelezwa kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya sekta ya nishati nchini.

Pia wameelezwa kuhusu jitihada za Serikali katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia pamoja na fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika sekta ya nishati.