The United Republic of Tanzania
Ministry of Energy

WANAWAKE WIZARA YA NISHATI WAS...

WANAWAKE WIZARA YA NISHATI WASHIRIKI SIKU YA WANAMKE DUNIANI.

Wanawake Wizara ya Nishati kutoka katika idara na vitengo mbalimbali wameungana na wanawake wote duniani kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, Wilayani Kongwa mkoani Dodoma.

Maadhimisho ya mwaka 2026 yanaongozwa na kauli mbiu isemayo: “Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana, Msingi Jumuishi Kufikia Dira 2050.”

Kwa umoja na mshikamano mkubwa, wanawake hao wamekusanyika kusherehekea na kutambua mchango wa wanawake katika maendeleo ya sekta ya nishati na taifa kwa ujumla.

Aidha, wameonesha dhamira ya kuendelea kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa kizazi chenye usawa, maendeleo na ustawi.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani hutoa fursa ya kuenzi juhudi, mafanikio na mchango wa wanawake katika nyanja mbalimbali za maendeleo, pamoja na kuhamasisha jamii kuendelea kuunga mkono usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake katika maeneo ya kazi na jamii kwa ujumla.

Katika maadhimisho hayo, mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule.