Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

WATALAAM KUTOKA BARA NA ZANZIB...

WATALAAM KUTOKA BARA NA ZANZIBAR WAKUTANA

Wataalam kutoka Wizara ya Nishati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na wa kutoka katika Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wamefanya kikao cha Ushirikiano kwa ngazi ya wataalam.

Kikao hicho cha Ushirikiano baina ya Wizara hizo kimefanyika Oktoba 27, mwaka huu katika ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo katika Mji wa Serikali jijini Dodoma.

Kikao hicho, kimeongozwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Nishati, Petro Lyatuu na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta na Gesi Asili Zanzibar (ZPDC), Mikidadi Rashidi na kuhudhiriwa na Wajumbe kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi zake pamoja na wajumbe kutoka katika Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi na Taasisi zilizopo chini yake.

Wajumbe wa kikao, walijadili ajenda mbalimbali ambazo ni hatua zilizofikiwa katika kukamilisha hati ya Mashirikiano(MoU) kati ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) na Mamlaka ya Udhibiti Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta Asilia, Zanzibar (ZPRA), hatua iliyofikiwa katika kukamilisha hati ya mashirikiano (MoU) kati ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta na Gesi Asili Zanzibar (ZPDC) na masuala mengine mbalimbali.

Wakati akifungua kikao, Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Nishati, Petro Lyatuu, aliwataka wajumbe hao kutoa michango yao kwa ufanisi.

Kikao hicho ni moja ya vikao ambavyo vinafanyika kwa kuzingatia muongozo uliotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais, ambavyo hupaswa kufanyika mara nne kwa mwaka.