WAZIRI NDEJEMBI AONGOZA KIKAO MAALUM KUIMARISHA USALAMA WA UPATIKANAJI WA MAFUTA NCHINI.
Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, Agosti 3, 2026 ameongoza kikao kazi cha pamoja na taasisi zinazoshughulikia sekta ya mafuta na gesi katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Nishati, jijini Dar es Salaam.
Lengo la kikao hicho lilikuwa kuweka mikakati madhubuti ya kuimarisha usalama wa upatikanaji na usambazaji wa mafuta nchini, sambamba na kuendelea kuhakikisha nchi inakuwa na akiba ya kutosha ya mafuta katika kipindi hiki cha mgogoro wa vita ya Mashariki ya kati kuliko pelekea kufungwa kwa mlango bahari wa Hormuz na changamoto zinazoendelea kujitokeza katika soko la kimataifa.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi, Dkt. James Mataragio; Kamishna wa Mafuta, Bw. Godluck Shirima; Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Bw. Salum Mnuna; Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Bw. Mussa Makame; Mkurugenzi Mtendaji wa PBPA, Bw. Erasto Simon; pamoja na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na taasisi zake.