Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

WIZARA YA NISHATI ENDELEENI KU...

WIZARA YA NISHATI ENDELEENI KUWEZESHA UWEKEZAJI WA VITUO VYA MAFUTA VIJIJINI- SIMBACHAWENE

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene ameiasa Wizara ya Nishati kuendelea kuweka mazingira wezeshi yatakayowezesha uwekezaji zaidi wa vituo vya mafuta vijijini.

Simbachaene amesema hayo tarehe 17 Juni, 2025, jijini Dodoma wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Nishati katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali ambayo leo yamefunguliwa rasmi

" Wafanyabiashara wengi wanataka kuwekeza kwenye vituo vya Mafuta vijijini kwakuwa bado kuna uhaba wa vituo, hivyo angalieni masharti yanayowekwa kwenye uwekezaji yasiwe kikwazo kwenye huduma hii muhimu." Amesema Simbachawene

Pia, Simbachawene ameishauri Wizara kuongeza kasi ya upatikanaji wa Nishati Safi ya Kupikia Vijijini pamoja na kuhamasisha uwekezaji kwenye Nishati Safi ya Kupikia.

Vilevile, ameipongeza Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuendelea kutoa huduma za Nishati kwa wananchi.