NISHATI SAFI YA KUPIKIA FIKENI VIJIJINI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akitoa maelekezo kwa wasambazaji wa Teknolojia ya Nishati Safi ya Kupikia kuhusu kuhakikisha Teknolojia hizo zinafika maeneo ya vijijini wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba na uzinduzi wa mpango wa ufadhili wa uunganishaji umeme kwa wananchi kati ya TANESCO na CRDB, uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, Kulia kwa Makamu wa Rais ni Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera.